Rais wa Ukraine ameviambia vyombo
vya habari vya magharibi, kuwa taifa lake kwa sasa lipo katika vita
halisi na Urusi, hivyo Ukraine haina budi kukabiliana kivita na
Urusi.
Rais Petro Poroshenko amenukuliwa
akisema hamuamini kabisa rais Vladimir Putin wa Urusi, licha ya kuwa
hana namna zaidi ya kuendelea kujadiliana naye.
Kwa upande wake Urusi imekuwa
ikikanusha tuhuma za mataifa ya magharibi kuwa amekuwa anatuma vikosi
vyake na silaha kuwasaidia waasi wa mashariki mwa Ukraine.
Umoja wa Mataifa umesema watu
wapatao 6,000 wameuwawa tangu kuanza kwa mapigano mashariki mwa
Ukraine Aprili 2014.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni