Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
amesisitiza kugombea tena urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi
uliopangwa kufanyika mwezi Juni, na kugomea shinikizo la jumuiya ya
kimataifa la kumtaka asigombee tena.
Licha ya kuwepo maandamano ya
kupinga asigombee tena urais, rais Nkurunziza amesema iwapo wananchi
wa Burundi wanamuamini, hii ni fursa yake ya mwisho kugombea urais
kama ilivyoamuliwa na mahakama ya Katiba.
Makumi ya watu wameuwawa na wengine
kadhaa wameuwawa tangu mwishoni mwa mwezi Aprili, wakati chama tawala
cha CNDD-FDD kilipo mteuwa Nkurunziza kuwania tea urais na kuibua
maandamano makubwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni