.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Mei 2015

UMOJA WA WANAWAKE WA CCM ( CWT ) WAMTAKA MH AMOS MAKALLA AWANIE KWA MUHULA MWINGINE UBUNGE JIMBO LA MVOMERO, WAMCHANGIA HELA ZA KUCHUKULIA FOMU HUKU WAKISEMA NI JEMBE

Wananachi wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro wakimlaki mbunge wao, Mh Amos Makalla alipofika ukumbini kuzungumza nao.
Umati uliofurika ukumbi wa Mabao- Mtibwa ukimshangilia mbunge wao Mh Amos Makalla alipowasili kuzungumza nao.                                          Mh Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa jimbo lake
Mh Makalla akiwahutibia wanawake wa matawi 10 ya UWT katika jimbo lake la Mvomero.
 
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla ameendelea kuchangiwa fedha za kuchukua fomu za ubunge na kampeni kutoka makundi mbalimbali wilaya ya Mvomero, na safari hii ni Umoja wa Wanawake wa Ccm (UWT) tawi madizini na kushirikisha matawi kumi kata ya Mtibwa na kata ya Diongoya.
 

Katika mkutano mkubwa wa kihistoria, wanawake wa matawi hayo walimtaka mbunge wao wakati ukifika achukue fomu na wao wanamuhaidi ushindi ndani ya chama na nje ya chama.
 

Akisoma risala kwa niaba ya akina mama hao, Katibu wa tawi Jumuiya ya Wanawake Tawi la Madizini, Bi Mariam Mdabwa, alieleza kuwa Mbunge wao amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia akinamama wajasiriamali, Vijana na kuboresha huduma za Afya, elimu, umeme na maji katika jimbo la Mvomero, hivyo umoja wa wanawake unakuomba uchukue fomu na kukabidhi fedha tasilimu shilingi 150,000 za kuchukulia fomu.
 

Akijibu risala hiyo, Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mh Amos Makalla aliwashukuru na kuwahaidi muda ukifika atachukua fomu, na pia aliwashukuru kwa mchango wa Fedha na kueleza awali alichangiwa fedha kiasi cha shilingi  2,309,000 na wananchi katika mkutano wa hadhara ukifanyika kijiji cha Manyinga.
Umati wa wanawake wa matawi 10 ya UWT wakimsikiliza mbunge wao wa jimbo la Mvomero, Mh Amos Makalla katika ukumbi wa Mabao- Mtibwa
Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akitabasamu baada ya kupokea mchango wa Fedha za kuchukua fomu za kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.
Naibu Waziri Maji na Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akionyesha mchango aliochangiwa na UWT Madizini kwa ajili ya fomu ya ubunge.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni