.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 1 Mei 2015

UZINDUZI WA KITABU CHA KUJIFUNZA KILINGALA CHA TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA KAVASHA CLUB

Jumapili hii tarehe 03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa atazindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.

Ni kitabu cha "Jifunze LINGALA kwa Kiswahili".

Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).

Ni ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi saa 3 jioni. MRC ndio ukumbi ambao "Club Raha Leo Show" ya TBC1 ilikuwa inafanyikia.

Tshimanga Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. 

Kwa hapa Tanzania amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis. Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.

Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni