Wajumbe 209 wa mkutano mkuu wa
Shirikisho la Soka Duniani Fifa leo wanatarajiwa kupiga kura ya
kumchaguwa rais mpya wa Shirikisho hilo huko jijini Zurich, nchini Switzerland wakati shirikisho hilo
linakabiliwa na kashfa nzito ya rushwa.
Rais wa shirikisho hilo la soka
duniani Fifa Sepp Blatter anawania kuliongoza shirikisho hilo kwa
muhula wa tano na anapambana na Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan ambaye anawania nafasi hiyo.
Uchaguzi huo unafanyika siku mbili
baada ya maafisa saba waandamizi wa shirikisho hilo kushikiliwa
jijini Zurich katika uchunguzi wa tuhuma za kugushi unaofanywa na Serikali ya Marekani na kutaka
watuhumiqwa hao kumi na nne kupelekwa nchini Marekani kufunguliwa
mashitaka.
Blatter na Prince Ali wanatakuwa na
muda wa dakika 15 kuhutubia mkutano mkuu wa baraza la shirikisho la
soka duniani Fifa ambapo kila mjumbe kati ya wajumbe 209 wa mkutano huo ana haki ya kupiga kura
katika uchaguzi huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni