Na woinde shizza ,Arusha
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church
Eliud Isanja amewataka Watanzania
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili
kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta
maendeleo ya taifa.
Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na
badala yake waitumie fursa hiyo
itakayoleta mabadiliko
yanayotarajiwa na wengi.
Akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo
ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa
wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza
taifa hili” Alisema Isanja
Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni
wa heshima katika mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea
wanaowagawa Watu kwa misingi ya ukabila na udini na kutowachagua kwani wataathiri umoja na mshikamano wa
kitaifa.
Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania
kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo
pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa tunapoelekea katika
uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa Tayari
zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na linategemewa
kukamilika nchini kote ili kukamilisha
uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza
tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni