.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 23 Juni 2015

BALOZI SEIF NA MKEWE MAMA ASHA WAJUMUIKA KATIKA FUTARI NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU HUKO PEMBA

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman akitoa neno la shukrani mara baada ya futari ya pamoja iliyowajumuisha waumini na baadhi ya wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Sheikh Khamis Kombo Ali kwa niaba ya wenzake akimshukuru Balozi Seif kwa hekima na imani yake ya kuwakusanya katika ibada ya futari ya pamoja iliyofanyika Hifadhi Hoteli Chake chake Pemba.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu aliofutari nao pamoja katika Hoteli ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Chake chake Pemba.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu aliofutari nao pamoja katika Hoteli ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Chake chake Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Wete Nd. Hassan Khatib Hassan aliyewahi kuwa Mkurugenzi Idara ya Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiagana na Balozi Seif baada ya futari hiyo.

Picha na - OMPR – ZNZ.

Wakati Waumini wa Din i ya Kiislamu Nchini wakiendelea kutekeleza Ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndani ya Kumi la mwanzo la Rehema upatikanaji wa bidhaa za vyakula katika masoko mbali mbali hapa Nchini unaonekana kuwa mgumu kutokana na ukali wa bei ya bidhaa tofauti.

Mfumko huo wa bei umekuwa ukiwapa mtihani mkubwa waumini hao wakati wanapohitaji kukunua bidhaa hizo licha ya wosia uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al – Hajj Dr. Ali Mohammed Shein wakati wa kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa
kuwaomba wafanyabiashara Nchini kuacha tabia ya kupandisha bei bidhaa zao ndani ya funga ya Ramadhani.

Hata hivyo waumini katika maeneo mbali mbali Nchini wameanza na utaratibu wao wa kujumuika katika futari ya pamoja ambayo huleta mapenzi na mahaba miongoni mwa waumini hao na kutiliwa mkazo na maswahaba wa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad { SAW }.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi walijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na baadhi ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Kisiwa cha Pemba kwenye Futari ya pamoja iliyowakutanisha katika Hoteli ya Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii { Hifadhi Hoteli } Tibirinzi Chake chake Pemba.

Akizungumza mara baada ya futari hiyo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman alisema Ramadhani ni Mwezi wa neema unaowakutanisha waumini na watu tofauti kubadilishana mawazo katika njia ya amani, upendo pamoja na Umoja.
 
Mh. Omar aliwashukuru Waumini na Wananchi hao kwa uamuzi wao wa kuacha vyakula na familia zao na kukubali kushiriki katika kitendo hicho ambacho huridhiwa na kupendwa na mola wa viumbe vyote Mwenyezi Mungu
Subhanahu wataala aliyefardhisha ibada hiyo ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramdhani.

Naye Sheikh Khamis Kombo Ali kwa niaba ya Waumini na Wananchi hao wamemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sei Ali Iddi kwa imani yake ya kuwaandalia futari hiyo akionyesha wazi kwamba ni kiongozi wa Wananchi.

Sheikh Khamis Kombo Ali alimtakia Balozi Seif na familia yake kheir, mafanikio na baraka katika maisha yake yajayo ambayo wanayatarajia kufaidika nayo katika miaka mengine ijayo.

Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa Nguzo Tano za Kiislamu zinazomuwajibikia kila Muumini wa Dini ya Kiislamu kuzitekeleza ikitanguliwa na Kuamini kwa moyo na kutamka kwa ulimi uwepo wa Mola Mtukufu, Kusali sala Tano, kutoa zaka pamoja na kwenda kuhiji Maka kwa muumini mwenye uwezo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni