Akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao maana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia wengine tupo mikoani tunafanya mazoezi tu bila kujipima viwango vyetu.
Hivyo napenda kutoa wito kwa mapromota kujitokeza kutusapoti sisi mabondia wa mkoani ili nasi tujipime na mabondia mnao waamini
Amesema kuwa, "najiamini kuwa naweza kazi, hivyo nami wasinikwepe kwa kuwa nawataka mabondia wao nasikia Bagamoyo Mkoa wa Pwani nao wanandaa ngumi mara kwa mara wajaribu kutuita na sisi si Dar peke yake mabondia wapo nchi nzima hivyo mapromota kama wana nia kweli ya kukuza mchezo na kuendeleza ngumi chini wawe wanachanganya mikoa mbalimbali, alisisitiza Kazaula.
Bondia huyo mwenye makazi yake Morogoro hakusita kumpongeza kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sapoti anayotoa kwa mabondia mbalimbali na kuwapatia vifaa vya masumbwi kwa gharama nafuu na DVD zenye mbinu mbalimbali za mafunzo ya ngumi anazotoa kuelekeza mabondia chipkiz ambao wana kiu ya kuwa mabingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni