Hukumu ya kesi inayowakabili
aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona pamoja, aliyekuwa
Waziri wa Fedha Basil Mramba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina Gray
Mgonja imeahirishwa kutolewa hii leo kufuatia jopo la mahakimu watatu
wanaosikiliza kesi hiyo kutotimia.
Akiahirisha hukumu hiyo
inayowakabili viongozi hao wa zamani wanao shtakiwa kwa matumizi
mabaya ya fedha za serikali wakati wakiwa madarakani, Hakimu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, John Lutamwa amesema hukumu ya kesi
hiyo sasa itatolewa Julai 3, mwaka huu kufuatia Hakimu Sauli Kilemela
kuwa Dodoma kwa shunghuli za kikazi.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na
mashitaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia
serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa
kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya MS Alex Stewart ya
Uingereza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni