Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23
watakaoondoka leo jioni kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka
kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
Akiongea na waandishi wa habari, kkocha
Mart Nooij amesema watatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa
Misri, vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana
kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania
unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini
Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa
Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11
jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili
jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini
Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi
Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey
Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda,
Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji
Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho
Ngasa na Juma Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick
Nyange “Kaburu”.
Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji ya
TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa
ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.
Kikosi kingine cha timu ya Taifa
kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwanda kucheza
mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya
mauaji ya Kimbali.
Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi
cha wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa
kirafiki, akisaidiwa na kocha Bakari Shime.
Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni
Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan
Isihaka, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa, Atupele
Green, Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu,
Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemba na Mohamed
Hussein.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni