Mataifa ya Singapore na Malaysia
katika jimbo la Sabah yanaadhimisha kwa siku moja ya kumbukumbu ya
watu waliokufa katika tetemeko la ardhi kwenye Mlima Kinabalu.
Watu 16 wamethibitishwa kufa baada
ya tetemeko hilo lililotokea Ijumaa, ambalo athari zake kubwa
zilikuwa katika eneo la Sabah.
Miongoni mwa watu sita waliokufa ni
watoto wa Singapore waliokuwa kwenye safari wakiwa na mwalimu wao
pamoja na muongozaji kupanda mlima.
Katika taifa la Singapore, bendera
zimepeperushwa nusu mlingoti, ambapo watu waliokusanyika kwe uwanja
wa michezo wa Asian walinyamaza kwa dakika moja kuwakumbuka
waliopoteza maisha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni