.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Juni 2015

MAANDALIZI YA SIKUKUU YA EID EL FITR CHAKECHAKE

BIASHARA ya Nguo za Mitumba kama vile shati na Suruali zimekuwa zikishika kasi katika kuelekea skukuu ya Eid el-fitr, pichani wananchi wakichagua nguo hizo, katika eneo la wazi mkabala na TRA,ZRB Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
IKIWA skukuu ya Eid El-Fitr inakaribia wananchi mbali mbali kisiwani Pemba, wamekuwa wakiwatafutia watoto wao nguo kwa ajili ya skukuu hiyo, kama walivyokutwa mbele ya soko la matunda Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
ENEO ambalo lilikuwa likitumiwa kwa ajili ya kuegesha vyombo vya moto maarufu Juwa kali, kwa sasa eneo hilo limekuwa likitumiwa kwa kufanya biashara za nguo katika kipindi hichi cha kuelekea Skukuu ya Eid El-Fitr.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BIASHARA ya Viatu vya wanaume katika kuelekea skukuu ya Eid El-Fitr vimepanda bei maradufu, ambapo kwa sasa kiatu kinauzwa kati ya shilingi Elfu 30,000/= hadi Elfu 28,000/=katika kipindi hiki.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BIASHARA ya nguo za kiume za watu wazima nazo pia zimekuwa bei juu, ambapo flana inauzwa kati ya shilingi Elfu 20,000/= hadi Elfu 22,000/= pichani kijana akijisajili kuipokea flana hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.) Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni