Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na kuwataka mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa uondoshaji wa Himaya moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika kwani mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana mpaka sasa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Naibu Kamishna wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya.
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakimsikiliza Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Habari Picha Na Hassan Silayo-MAELEZO
Mawakala wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza kutumika hivi Karibuni.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika.
“Sasa tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza kutokea”. Alisema Bw. Kabisi
Bw. Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala waliojisajili mpaka sasa.
Aidha Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali.
Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha.
Pia Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza katika makusanyo ya mapato ya serikali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni