.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 15 Juni 2015

MHE MAKALLA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGANGO CHA LANGALI PAROKIA YA MGETA AMBAPO JUMLA YA MILIONI 12 ZILIPATIKANA

 Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akiongea wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Langali, Parokia ya Mgeta. 

Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla leo ameongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa kigango cha Langali Parokia ya Mgeta. 

Katika harambee hiyo, jumla ya Fedha zilizopatikana ni shilingi milioni 12, na mgeni rasmi Mhe mbunge wa jimbo la Mvomero Amos Makalla akichangia shilingi milioni moja laki tano.
 

Aliwataka waumini na wananchi kujenga tabia ya kumtolea Mungu, kwani kila tulichonacho ni mali ya Mungu.
 

Amewawaeleza umuhimu wa waumini kujitoa kwa moyo ili kujenga kanisa ambalo kitasaidia kufanya ibada kijijini hapo badala ya kwenda mbali kijiji cha jirani.
                                                          Waumini waliojitokeza katika harambee hiyo.
 Mbunge wa jimbo la Mvomero, Mh Amos Makalla akipokewa na waumini wakati alipofika kushiriki harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Langali, Parokia ya Mgeta.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni