Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita.
Komredi Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wilayani Geita, ambapo aliwadhihaki wapinzania kwamba watashindwa vibaya katika uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu akidfai hawana sera wala mipango inayoeleweka ya kuwasaidia watanzania kupiga hatua za kimaendeleo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Sehemu ya umati wa watu waliofurika katika mkutano wa hdhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.
Wananchi wa Kijiji cha Shinyamwendwa, Kata ya Nyanguku wakitoa malalamiko yao baada ya kuzuia msafara wa Komredi Kinana,kuhusu ubovu wa barabara, kutopatikana kwa mawasiliano katika Kijiji hicho, katika Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.
Komredi Kinana akilakiwa na wananchi wa Kijiji cha Nyankanga ambapo alishiriki kulima barabara ya Kijiji wilayani Geita, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Busanda.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Geita, Vick Kamata akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Nyankanga, Jimbo la Busanda mkoasni Geita leo.
Mwandishi wa Habari wa Clouds TV, Salum Mwinyimkuu, akiwaonesha wasanii picha mbalimbali alizowapiga walipokuwa wakitumbuiza wakati msafara wa Komredi Kinana ulipowasili katika Kijiji cha Nyankanaga, Jimbo la Busanda, Mkoa wa Geita. Kutoka Kulia ni Manaeno Richard 'Ngembele' na Sadick Malehiwa.
Komredi Kinana (wa tatu kulia), akishiriki kulima barabara ya Kijiji cha Nyankanga, wilayani Geita wakati wa ziara yake katika Jimbo la Busanda.
Sehemu ya eneo la machimbo ya Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico ambalo lina mgogoro na wachimbaji wadogo wadogo ambalo Komredi Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni