Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gamaakisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana iongozi wengine wakiskilizanyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakatiwa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika laHifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi zaTaifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olelewakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na TANAPA.
Na Dixon Busagaga wa Globu aya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni