Mkuu wa usalama wa Rwanda Karenzi
Karake, ambaye alikuwa akihitajiwa nchini hispania kwa makosa ya
uhalifu wa kivita amekamatwa jijini London.
Polisi wa nchi hiyo wa kitengo cha
kubadilishana uhalifu wamemkamata Jenerali Karake, katika uwanja wa
ndege wa Heathrow siku ya jumamosi, imefahamika hii leo.
Jenerali Karake mwenye umri wa miaka
54, atabakia kizuizini hadi siku ya alhamis, baada ya kufikishwa
kwenye mahakama ya westminster.
Jenerali Karake anatuhumiwa kuagiza
mauaji wakati akiwa mkuu wa intelejensia katika jeshi wakati wa
machafuko ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni