Watu wapatao 20 wameuwawa baada ya
mwanamke aliyejitoa mhanga kwa bomu kushambulia soko la samaki
kaskazini mashariki mwa mji wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mshambuliaji huyo mwanamke
alijifanya kuwa ni ombaomba wakati akiingia katika soko hilo kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo.
Mwanamke huyo alijilipua ndani ya
soko huku mwingine akikimbia baada ya kulipua fualana yake yenye
mabomu karibu na soko lakini mlipuko wake haukuleta madhara. Kundi la
Boko Haram halijaeleza lolote kuhusiana na shambulio hio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni