Mwanamke mmoja amefikishwa
mahakamani nchini Ufaransa kwa tuhuma kuendesha njama za kujipatia
mamilioni ya euro nchini Chile kwa kutengeneza jibini ya miujiza kwa
ajili ya urembo kwa wanawake.
Mwanamke huyo Gilberte van Erpe, 74,
anatuhumiwa kuuza jibini hiyo feki isiyo thamani yoyote kwa
kuchanganya mkorogo na poda ya kawaida na kuiuza kwa bei kubwa.
Wauzaji wajumla walishawishiwa
kuiuza bidhaa hiyo feki kwa wingi, kutokana na kupatiwa sehemu ya
faida kutokana na mauzo.
Mwanamke huyo alichuma kiasi cha
dola milioni 16.14 na kuweka historia ya utapeli mkubwa kuwahi
kutokea nchini Chile.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni