.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 7 Juni 2015

NAIBU WAZIRI WA MAILIASILI NA UTALII,MOHAMED MGIMWA AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA KILIFAIR 2015.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Moshi Club kwa ajili ya kufungua rasmi maonesho ya kimatifa ya Kitalii yajulikanayo kama KiliFair 2015.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akisalimiana na Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Utalii na Michezo wa Zanzabar Bi Hindi Khamis walipokutana katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo,Naibu waziri wa utalii,Mohamed Mgimwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine akiwemo kaimu mkuu wamkoa wa Kilimanjaro,Dkt Charles Mlingwa,katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa,Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufunguro.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akiwa ameambata na naibu waziri wa habari,utamaduni ,utalii na Michezo Zanzibar,Bi Hindi Khamis alipokuwa akitembelea banda la maoensho ya utalii la Zanzibar.
Naibu Waziri ,Mgimwa akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya utalii ya Zara tour
Naibu Waziri ,Mgimwa akinywa kahawa alipotembelea banda la kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines.
Waoneshaji wengine walibuni mbinu zaidi wakiwatumia wafugaji jamii ya maasai katika maonesho hayo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA,Erastus Rufunguro akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Asante Tour ,Cuthbert pamoja na mkurugenzi wa Kilifair ,Tom.
Naibu waziri Mgimwa akizungumza na Cuthbert.
Naibu Waziri wa maliasili na utalii akisalimiana na Meneja Biashara wa kampuni ya Kibo Palace ,Charity Githinji ,wakati Naibu waziri alipotembelea banda hilo.
Baadhiya wafanyakazi wa kampuni ya Kibo Palace wakiwa katika banda lao la maonesho
Naibu waziri wa utalii Zanzibar Bi Hindi akipokea zawadi toka Kibo Palace.
Manaibu waziri wa utalii,Tanzania bara na
Zanzibar,Mgimwa na Bi Hindi wakiwa katika picha ya pamoja na
wakurugenzi wa Kilifair Dominic Shoo na Tom.
Mkurugenzi wa kampuni ya Kilifair ambao ndio
waandaji wamaonesho hayo ,Dominic Shoo akizungumza wakati wa ufunguzi
wa maonesho hayo .
Naibu waziri wa habari,utamaduni,utalii na
Michezo Zanzibar ,Bi Hindi Khamis akizungumza wakati wa ufunguzi wa
maonesho hayo.
Baadhi ya wageni waliofika kwa ajili ya
maonesho hayo.
Naibu Waziri ,Mgimwa akitoa hotuba yake ya
ufunguziwa maonesho ya kimataifa ya utalii ya Kilifair 2015
yanayofanyika katika viwanja vya Moshi Club.
Viongozi wakiwa katika picha ya
pamoja.
Naibu waziri Mgimwa akiteta jambo nammoja wa
wakurugenzi wa kampunu ya Kilifair Dominic Shoo.
Kikundi cha burudani toka nchini Kenya
kikitoa burudani katika maonesho hayo.
Baadhi ya mabanda yaliyopo ndani ya viwanja
vya Moshi Club yakionesha bidhaa na huduma zitolewazo na kampuni
mbalimbali za utalii.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Kanda ya Kaskazini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni