Kuendelea kwa kesi inayowahusu
wachungaji wawili Jijini Khartoum, kunaendelea kuonyesha historia ya
Sudan ya unyanyasaji wa makundi madogo ya watu wenye imani tofauti.
Wachungaji hao Yat Michael na Peter
Yen wamefunguliwa mashtaka tofauti yakiwemo ya kudharau mfumo wa
Katiba, kuanzisha vita na serikali pamoja na kuchunguza siri za
serikali.
Mashtaka ya kwanza mawili
yanayowakabili wachungaji hao, adhabu yake ni hukumu ya kifo.
Kesi yao imeligusa kundi la Kampeni
la Kikristo nchini Marekani ambalo limesema wachungaji hao
wanashtakiwa kutokana na imani yao ya Kikristo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni