Shule ya Sekondari ya Kalwana
inayohudumiwa na serikali na kanisa katika wilaya ya Mubende nchini
Uganda imefungwa kwa muda, kufuatia ghasi za wanafunzi ambao
wanawatuhumu walimu wao kujihusisha na vitendo vya ushirikina.
Vikosi vya kupambana na ghasia
vimewekwa kuzingira majengo ya shule hiyo ya bweni na ya kutwa ili
kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayerejea kwa sasa.
Wanafunzi wa shule hiyo waliandamana
na kuwafungia walimu wao kwenye ofisi zao kwa madai kuwa tangu waanze
muhula huu wa masomo wamekuwa wakikabiliana na vitendo vya
kishirikina.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni