Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni