Na Mwandishi Wetu.
Chama
cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi
wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya
filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi
ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa
hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu
Vilevile
wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi
nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu
wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile
zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012
ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa
na kupewa daraja.
Kutokana
na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na
kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu
kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo
walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili
ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka
filamu sokoni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni