.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Juni 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,LAZARO NYALANDU AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WANANCHI KUNYANYASWA

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo katika ziara ya siku moja kuzungumza na wananchi baada ya mwananchi mmoja kuuawa kwenye msitu wa Marang unaohifadhiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa(Tanapa).Waziri Nyalandu ameunda Tume ya kuchunguza mgogoro huo ambayo itatoa mapendekezo serikalini kwa utekelezaji.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na mmoja wa wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo baada ya kuhutubia wananchi hao na kuwahidi serikali kuwachukulia hatua askari waliokiuka taratibu za maadili.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha,Cesilia Paresso akihutubia wananchi wa Kata ya Buger na kuitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuzingatia sheria na wananchi kulinda Msitu wa Marang kwaajili vizazi vijavyo.
Mkazi wa Kata ya Buger,Rehema Tango akitoa kero zake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni