Na Dotto Mwaibale
KAIMU Mkurugenzi Mwendeshaji, bodi ya Utalii nchini, Devotha Mdachi, alisema ufinyu wa bajeti ya matangazo katika sekta ya utalii unasababisha sekta hiyo, kutofanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine.
Mdachi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akitolea
ufafanuzi wa onesho la utalii nchini, linalotarajia kufanyika Oktoba mosi hadi 3 mwaka huu linalojulikana kama Sites.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa bajeti finyu iliyotengwa na Serikali katika kutoa matangazo ya utalii wa ndani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine zinavyojitangaza duniani.
Pia, alisema kutokuwa na ofisi za bodi ya utalii katika kila mkoa
na kutokuwa na Shirika la Ndege la Taifa kusababisha utalii wa ndani kuwa mdogo.
“Wenzetu wa Kenya bajeti yao ya matangazo ya utalii ni kubwa
ukilinganisha na sisi kwani wao wametenga bilioni 36 katika
matangazo, lakini sisi bajeti yetu ya matangazo ni finyu sana ambapo ni bilioni 2.3,” alisema Mdachi
Kwa upande wake, Meneja huduma za utalii nchini ambaye
pia ni Mratibu Mkuu bodi hiyo, Sebastian Philip alisema onesho hilo litakutanisha wafanyabishara wa hapa nchini kutoka kwenye masoko ya utalii, hivyo ni vema watanzania kutumia fursa hiyo kuhakikisha kunaleta soko kubwa la utalii nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni