BONDIA Mohamed Matumla anatarajia kupanda tena uringoni siku ya Idi pili katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani kupambana na Koba Nodat katika uzito wa KG 57 mpambano wa raundi sita.
Matumla anapambana mpambano huo baada ya mpambano wake wa mwisho kumtwanga Mchina kwa point.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.
Mratibu na promota wa mpambano huo Muhsin Sharif amesema mbali na mpambano uho, kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi.
Bondia Iddi Pialali kutoka Kiwangwa Bagamoyo atapambana na Mesharck Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano wa raundi nane kg 66, wakati bondia machachari katika tasnia ya mchezo wa masumbwi nchini Vicent Mbilinyi atavaana na Khalidi Hongo mpambano wa raundi nne wakati Twalibu Tuwa atavaana na Sudi Sudi.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni