Na Woinde Shizza,libeneke la kaskazini blog
Mwendesha magari Randeep Shingh kutoka jijini Dar es Salam ameibuka mshindi katika mashindano ya kila mwaka ya mbio za nyika za magari nane-nane rally yaliyotimua vumbi katika mji wa Arusha mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yamefanykia kwa siku mbili mfululizo huku yakishuhudiwa ushindani mkali kwa madereva hao waliotoka mikoa mbalimbali na Randeep Shingh akiwa na msoma ramani guvinder singh wa gari ya mistubish lancer akiibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.
Katika mashindano hayo yaliyokuwa yakitofauti mwaka huu, baada ya kufungiwa mitambo ya kisasa ya kidigitali kwa kila gari ili kuwezesha ufuatiliwaji wa kila gari na njia zitakazopitia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hakuna zengwe wala suala la madereva kuiba njia na hata kupotea porini.
Zaidi ya madereva 20 kutoka ndani na nje ya nchi walioshindana zaidi ya Km 198 huku mshindi wa pili akiwa ni Raj Pal Dhani na msoma raman Sinder Sudle wakiwana na ghari la subaru impreza nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na Gurjit Singh .
Huku dereva mkongwe wa nchini tanzania Gerald Miller akiambulia nafasi ya sita, HUKU baadhi ya madereva walioshiriki katika mashindano hayo wakisema yalikuwa magumu mwaka huu huku wengine wakizungumzia changamoto ya barabara
Baadhi ya mashabiki wa mchezo waliojitokeza kwa wingi kutazama mashindano ya hayo ya utrack nanenane rally walisema wamefurahi na kuiomba serikali kuwezesha mashindano haya kufanyika mara kwa mara
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni