Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amejibu mapigo dhidi ya kauli ya mke wa Rafa Benitez, aitwae Montse,
baada ya kusema kuwa mumewake amekuwa akisafisha makosa ya Mourinho
katika klabu alizofundisha.
Mourinho amekanusha tuhuma hizo huku
akimtupia dongo Banitez kuhusiana na kuongezeka uzito na kumtaka mke
wake amsaidie mumewe kupunguza unene.
Kocha huyo wa Chelsea amesema
mwanamke huyo amechanganyikiwa kwani mumewe alienda Chelsea kuchukua
nafasi ya Roberto Di Matteo na alijiunga na Real Madrid kuchukua
nafasi ya Carlo Ancelotti na wala si iliyoachwa na Mourinho.
Kocha Rafa Banitez akiwa na mkewe Montse
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni