Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Sheikh Hassan Hussein (Nyundo), baada ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya Masheikh mbali mbali, nyumbani kwake Mbweni
Baadhi ya Masheikh wakiongozwa na Mufti Mkuu (wa tatu kushoto) na Kadhi Mkuu (wa nne), wakijiandaa kwa ajili ya sala ya Magharibi kabla ya futari, nyumbani kwa Maalim Seif Mbweni.
Baadhi ya Masheikh na waumini wa dini ya Kiislam, wakijumuika pamoja katika futari iliyoandaliwa na Maalim Seif nyumbani kwake Mbweni.
Masheikh wakiitikia dua baada ya sala ya magharib nyumbani kwa Maalim Seif Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya Masheikh na waumini wa Kiislamu wakisikiliza mawaidha yaliyotolewa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani), nyumbani kwa Maalim Seif Mbweni Zanzibar (Picha na Salmin Said, OMKR)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni