.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Julai 2015

MAALIM SEIF ATUMA SALAAM ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS MSTAAFU WA INDIA


                                                                                        Na Khamis Haji (OMKR)
 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa India kufuatia kifo cha mwanasayansi aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Dk. Avul Pakir Abdul Kalam kilichotokea Jumatatu iliyopita.
 

Ametuma salamu hizo wakati alipozungumza na Balozi mdogo wa India hapa Zanzibar, Satendar Kumar huko katika ofisi za Ubalozi huo Migombani, ambapo Maalim Seif alifika kusaini kitabu cha maombolezi.
 

Maalim Seif amesema Kiongozi huyo ni msomi aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa la India hasa kutokana na mchango wake katika uvumbuzi wa vyombo vya anga za juu, kwa ajili ya matumizi ya kiraia na Kijeshi.
 

Maalim Seif amesema bila shaka kifo chake kimeacha pengo na masikitiko makubwa sio tu kwa wananchi wa India, bali kwa jamii ya wasomi Duniani, na amewataka wananchi wa India kuwa na subira katika wakati huu mgumu wa maombolezi. 

Abdulkalam (83) ambaye alipewa jina la umaarufu ‘mtu wa misaili wa India’ alishika nafasi ya Urais wa India mwaka 2002 kwa muda wa miaka mitano.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni