.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 6 Julai 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF ASHIRIKI MAZIKO YA ALIYEKUWA SHEIKH ALAWY BIN OMAR BIN SALIM BAALAWY

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akielekea viwanja vya Ole Kanambe kwa ajili ya kushiriki sala ya aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
  Waislamu mbali mbali kisiwani Pemba, wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
 Waislamu mbali mbali kisiwani Pemba, wakiusalia mwili wa aliyekuwa sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu sheikh Alawy Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku. Amesaliwa katika viwanja vya Ole Kanambe.
 Waislamu mbali mbali kisiwani Pemba, wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu Kisiwani Pemba, wakiitikia dua baada ya kuusalia mwili wa aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe, marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu Kisiwani Pemba, wakiomba dua baada ya kuuzika mwili wa aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe, marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy. (picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad (OMKR)

Maelfu ya waislamu kutoka maeneo mbali mbali kisiwani Pemba wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, lao wamejumuika katika mazishi ya aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu Sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy.

Sheikh Alawy ambaye amezikwa hapo hapo Ole Kanambe, alifariki jana usiku akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mmoja kati ya watoto wa marehemu sheikh Alawy, Sheikh Mussa bin Alawy amesema mbali na marehemu huyo kuwa na darsa kubwa kutoka maeneo jirani, wanadarsa wengine walikuwa wakitoka maeneo ya mbali kisiwani Pemba yakiwemo Tumbe, Fundo, Kengeja na Mkoani kufuatilia darsa zake.

Sheikh Alawy aliyezaliwa mwaka 1934 akiwa Sheikh maarufu katika eneo la Ole Kanambe kisiwani Pemba na Zanzibar kwa ujumla, ameacha kizuka mmoja na watoto 12.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala Pema Peponi (Ammiin)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni