.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 4 Julai 2015

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO JIPYA LA TTCL PEMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Shirika la Simu Tanzania TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati alipowasili Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo Julai 3, 2015 kwa ajili ya Kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi za shirika hilo. Katikati ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Simu Tanzania, TTCL, wakati alipowasili kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi za Shirika hilo Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Julai 3,2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu ramani ya Jengo hilo la TTCL, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya 'Quality Buildin Contractors Ltd', Khamis Ally Shaibu, wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, iliyofanyika leo Julai 3, 2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa,akizungumza.
Mkurugenzi Shirika la Simu Tanzania TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura, akizungumza
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, Wilayani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, leo Julai 3, 2015
BAADHI ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL, wakimjuika na wananchi wa Pemba, kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la afisi ya kampuni hiyo, liliolopo Madungu mjini Chake chake kisiwani humo
VIONGOZI Wakuu wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba, ambapo wa kwanza ni mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla akiwa na mkuu wa mkoa mwenzake wa Kaskazini Mhe: Omar Khamis Othman wakifuatia kwa karibu utenzi ulioghaniwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la afisi ya TTCL Pemba
BAADHI ya wananchi na wafanyakazi wa serikali waliohudhuria kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la afisi ya kampuni ya simu ya TTCL, liliolopo Madungu mjini Chake chake kisiwani humo, wakimskiliza Makamu wa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania dk: Mohamed Gharib Bilali, kwenye hafla hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni