.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 6 Julai 2015

RAIS WA TFF AHUDHURIA KONGAMANO CANADA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi anashiriki katika kongamano la Fainali za Dunia kwa Wanawake zinazofanyika Vancouver- Canada kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 - 5 Julai mwaka huu.

Katika kongamano hilo Malinzi ameambatana na katibu mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma.

Kongamano hilo la soka la Wanawake linahudhuriwa na nchi 209 wanachama wa FIFA, ambapo hufanyika kila baada ya miaka minne, pindi zinapofanyika fainali za Dunia kwa wanawake.

Miongoni mwa wachangiaji wa kongamano hilo ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya FIFA, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha soka cha nchini Burundi, Lydia Nskera.

STARS YAALIKWA CHAKULA CHA JIONI UBALOZINI
 

Wakati huo huo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager jioni ya leo ilialikwa chakula cha jioni na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania iliyopo jijini Kampala.

Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, wenyeji wakiwemo maofisa wa ubalozi , watanzania waishio nchini Uganda waliwapongeza wachezaji, viongozi kwa mchezo mzuri dhidi ya Uganda na kuwatakia kila la kheri katika safari ya jumatatu ya kurejea jijini Dar es salaam.

Stats inatarajiwa kuwasili Dar es salaam uwanja wa Mwl. JK Nyerere jumatatu saa 10 kamili jioni kwa shirika la ndege la Rwanda.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni