Sanamu la mchekeshaji mkongwe Bill
Cosby limeondolewa katika eneo la bustani ya Disney, kufuatia
kubainika kuwa mchekeshaji huyo aliwahi kukiri mahakamani kumpa
mwanamke dawa za kumlevya kabla kulala nae.
Nyaraka za mahakama zilizotolewa
wiki iliyopita zimebaini kuwa Cosby alikiri mnamo mwaka 2005 kuwa
alikuwa na dawa aina ya Quaaludes kwa lengo la kuwapatia wanawake
kabla ya kulala nao.
Bill Cosby anakabiliwa na mfululizo
wa tuhuma za kuwabaka wanawake ambazo anadaiwa kuzitenda karibu
muongo mmoja uliopita.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni