Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imesema kuwa itaongeza muda wa siku nne tu wa kuandikisha wapiga
kura kwa wakazi wa Dar es Salaam, baada ya muda wa awali wa tarehe
31, kumalizika.
Akiongea na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva
amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa
ratiba zitaingiliana.
Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka
sasa watu zaidi ya milioni 18 wameandikishwa katika daftari la kudumu
la wapiga kura kwa njia ya mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni