Abbasi Mlanya Na yeremias
ngerangera , Tunduru MKutano Mkuu wa jumuiya ya Wanawake Tanzania
(Uwt) ya Chama cha mapinduzi WilayaninTunduru wamewachagua Madiwani
wa Viti maalum waatakao shirikiana na wagombea wa udiwani katika kata
zao.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo
uliofanyika katika ukumbi wa Sky way Mjini hapa, mjumbe wa mkutano
mkuu wa CCM mkoa wa Ruvuma aliyeteuliwa kusimamia uchaguzi huo
Bi.Awetu Matumla Akukweti alisema kuwa Tarafa ya Mlingoti washindi ni
Bi. Siwema kalipungu na Atingala Mohamed.
Alisema katika matokeo hayo
kalipungu alipata kura 380 kati ya kura 785 zilizo pigwa, Atingala
alipata kura 371 na kuwabwaga wapinzani wao Bibie mandingo ambaye
alipata kura 277, Fatuma kaisi kura 175, Rehema Machemba 121, Kanunu
Mgomba 94, Pendo Luwambano 54 na Asha mpinga 17.
Alisema tarafa ya matemanga washindi
ni Bi. Stawa Timamu alipata kura 799, Sharifa Niko 569 na kuwabwaga
Ashura Rashid kura 179, Amina Mpepo 174,Aha Kihenge 158, na Amina
Hokororo 153.
Kwa mujibu wa Akukweti, wajumbe hao
waliwachagua Bi. Zenna Wina kwa kura 478 na Dani Malikuseka kura 453
kuwa wagombea wa nafasi hiyo katika tarafa ya Namasakata na kuwabwaga
Bi awetu Ndeka kura 319 na Bi Rukia Makina aliyepata kura 187.
Katika tarafa ya Nalasi
aliochaguliwa ni Aindi Daruweshi aliyepata kura 713 na Alusi Unusi
kura 195 huku tarafa ya Lukumbule Alusi Ally akibuka kidedea kwa
kupata kura 564 na Hadija kazibule kura 508 na kuwabwaga Bi. Habiba
seph 338 na hadija Chipoka 226.
Kwa upande wa tarafa ya Nampungu
wajumbe hao Bi. Rehema Nyoni alibuka mshindi kwa kura 602 huku akiwa
anafuatiwa kwa na Bi.Hadija Napunda aliyepata kura 128 na tarafa ya
Nakapanya Bi. Maimuna Bora aliibuka mshindi kwa kupata kura 576 na
Fatuma Mapila 451 huku Hawa Machemba akishia kupata kura 308, Mwajuma
Kalesi 154, Perepetua Makina 87,Dorini Tindo 78, Sofia Hasan 74,
Mwanashungi Rashid 35
.
Awali akiongea na wajumbe hao katibu
wa Uwt wilaya ya tunduru Bi. Fatuma Mandingo aliwataka wajumbe hao
kutumia nafasi hiyo kwa umakini kwani endapo watafanya makosa kwa
kuchagua wagombea wabovu adhabu yao ni miaka 5.
Alisema hata kama wamekwisha pewa
fedha na baadhi ya wagombea hao, fedha hizo wale lakini wabakie na
msimamo wao wa kuchagua Wagombea wenye uwezo na kuongea kuwa “
akilizakuambiwa, waongeze na zao” Mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni