Kijana aliyemuua kwa kumchoma choma
kwa kisu mtoto wa kambo wa mchekeshaji mkongwe Morgan Freeman huko
Manhattan, jana asubuhi kwa imani za kumtoa majini imeelezwa kuwa ni
rafiki wa kiume wa binti huyo E'Dena Hines.
E'Dena Hines, 33, alikutwa akiwa
amekufa baada ya rafiki yake wa kiume Lamar Davenport, 30,
alipomshambulia kwa kisu nyumbani kwake Washington Heights, ambapo
Davenport alikutwa akiwa amesima kando ya mwili wake akipiga kelele'
Shetani toka'.
Kijana Davenport ambaye alikuwa
anapenda kuwa muigizaji ana historia ya kutumia dawa za kulevya,
amekamatwa na kupelekwa kituo cha afya cha Columbia Presbyterian
Medical Center, kufanyiwa vipimo vya akili yake.
E'Dena Hines kushoto akiwa na mpenzi wake Devenport kati kati


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni