.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 17 Agosti 2015

BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA MAASIFA WA BENKI YA DUNIA ( WB ) OFISINI KWAKE VUGA, ZANZIBAR


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo
haja kwa wakulima Nchini kupatiwa taaluma ya kutosha na ya kisasa
katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia Nchi yanayoonyesha muelekeo
wa kuiathiri Sekta ya Kilimo Duniani.
 
Alisema Taaluma hiyo inayohitaji uwezeshwaji mkubwa kwa lengo la
kufanikiwa vyema inapaswa kuungwa mkono ya Benki ya Dunia { WB } ili
kuwapa faraja wakulima wanaofikia Idadi ya asilimia 80% ya watu wote
Nchini Tanzania.
 
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Ujumbe wa
Maafisa wa Benki ya Dunia { WB } ukiongozwa na Mwakilishi wa Taasisi
hiyo hapa Tanzania Bibi Bella Bird alipokutana nao Ofisini kwake Vuga
Mjini Zanzibar.
 
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na
washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi inajitahidi kuimarisha
miundo mbinu katika sekta ya kilimo itakayowapa fursa pana wakulima
kuongeza uzalishaji hasa katika kilimo cha umwagiliaji.
 
Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa lazima liwe na chakula cha hakiba
ya kutosha ili kujiweka tayari na upungufu wowote unaoweza kutokea
kutokana na sababu za ukame, majanga na mabadiliko ya hali ya hewa.
 
Akizungumzia changamoto inayowakumba vijana wanaotumbukiza katika
matumizi ya dawa za kulevya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliuomba Uongozi huo wa Benki ya Dunia kuendelea kuisaidia Zanzibar na
Tanzania kwa jumla taaluma pamoja na uwezeshaji wa kuambana na janga hilo.
 
Balozi Seif alisema kwamba nyumba za kurekebishia tabia kwa vijana
walioathirika na dawa za kulevya zinahitaji gharama kubwa kisi kwamba
Serikali pekee haiwezi kumudu kuzihudumia.

 

Mapema Mwakilishi wa Benki ya Dunia { WB } Nchini Tanzania Bibi Bella
Bird alisema kwamba Taasisi yake imekuwa ikiangalia zaidi namna na
mbinu za kuwasaidia Vijana katika nchi mbali mbali Duniani kumudu
kuendesha maisha yao.
 
Bibi Bella Bird alisema hatua hiyo imelenga kuwakinga vijana
wanaomaliza masomo yao wasitumbukie katika majanga mabaya na badaya
yake wawe na maisha ya matumaini.
 
Alisema ipo baadhi ya Miradi inayosimamiwa na Benki ya Dunia Nchini
Tanzania ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana waingie
ndani ya dunia ya mpya ya sayansi na teknolojia kwa kujiamini.
 
Alifahamisha kwamba Vyuo vya kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya
sayansi na lugha ni miongoni mwa mikakati ya Benki hiyo katika
kuliandaa Taifa la Tanzania kuwa na wataalamu waliobobea katika fani
ya sayansi hapo baadaye.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni