.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 10 Agosti 2015

BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA KIDEDEA AFRIKA YA KUSINI

                                                                                               Na Mwandishi Wetu
 

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika Kusini baada ya kumdunda vibaya Lizbeth Sivhaga wa nchini humu.
 

Huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awali
 

Hata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili

Ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote
 

Bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne.
Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi
 
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni