Timu ya soka ya Arsenal imeanza vibaya ligi kuu England baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 toka kwa West Ham, katika mchezo uliochezwa uwanja wa Emirate ambao ni uwanja wa nyumbani wa Arsenal.
Langoni akiwa amesimama mlinda mlango, Petr Cech aliyesajiliwa kutoka Chelsea, Arsenal walishuhudia dakika 90 zinamalizika wakiwa wamelala nyumbani kwao.
Mabao hayo ya West Ham yaliwekwa kimiani na wachezaji Cheikhou Kouyate katika dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza, na bao la pili nala ushindi likafungwa na Mauro Zarate katika dakika ya 57 ya kipindi cha pili.
DUH NAANZA VIBAYA!! Mlinda mlango wa Arsenal, Petr Cech akiwa hana la kufanya zaidi ya kuangalia nyavu zikitisikia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni