Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa
kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi
kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki.
Takriban watoto 8
kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii
kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi
katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa
wengi sana.
Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati
wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa
bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo,
kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata
maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara.
Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha
unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo
linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida
zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha
‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa
wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko
upumuaji.
Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga
ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo
kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa
mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake
unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi
wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na
mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi.
Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G
Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara
ya Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona
kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio.
Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote
muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, kukata usambazaji wa
damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani.
Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana.
Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu
nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa
maisha.
Wakati mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya
awali ya kuchunguza hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya
kifua na ECG ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo
(ECG) mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa
ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu
yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, takwimu
hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia katheta ya moyo
na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.
Uboreshaji wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa
upasuaji kwa watoto. Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na
mwongozo wa pande tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii
inatoa mpango bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na
kwa hiyo matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.
Kuna tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya
hizi ni pamoja na mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa
kuufungua na kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na
hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya
moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa
vinavyowezesha kuipata mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na
valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii
mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa
katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka
zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.
Namna nyingine za
matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali mbaya zaidi ya moyo ni
ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani (upasuaji). Upasuaji huu unaweza
kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye
gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi
unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada
kutoka kwa timu.
Watu kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi
wanashiriki katika kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo.
Madaktari wa watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile
kudhibiti maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia
ya kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu zaidi
kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.
Kwa mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto
Apollo, Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza
kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) kupata
kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika kuchunguza moyo wa
mtoto akiwa ndani tumbo la mama.
Daktari bingwa wa
Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya ujauzito.
Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi sahihi juu ya
mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika katika moyo.
Njia nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa
kuepukana ndoa kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa,
na kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na kasoro
katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya kuepuka ugonjwa
wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa matibabu ya maambukizi
katika koo kwa wakati kwa kutumia
antibiotiki.
Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali
ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa
watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya
sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha
kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.
Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu
bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa
upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea
na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa
muda mrefu maishani bila matatizo.
Inachangiwa na:
Dk Neville A.G Solomon
Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu
Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni