.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 17 Agosti 2015

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UWAKILISHI JIMBO LA MAHONDA

Wanachama mbali mbali wa Vyama vya Siasa Nchini walioomba na
kuthibitishwa na vyama vyao kuwania nafasi mbali mbali za uongozi
wameanza rasmi kujitokeza kuchukuwa fomu za kuwania kugombea nafasi
walizoomba katika  Ofisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya.
 
Zoezi hilo litalowashirikisha wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na
Udiwani linatarajiwa kuendelea hadi Tarehe 6 Septemba 2015 ambapo
wanaochukuwa fomu hizo watalazimika kujaza vipengele vyote vinne
vilivyomo kwenye Fomu hizo.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa
miongoni mwa wanachama kadhaa wa Chama cha Mapinduzi waliojitokeza
kuchukuwa Fomu hizo ambapo yeye ameamuwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishgi Jimbo la Mahonda.
 
Balozi Seif alikabidhiwa fomu hizo mapema asubuhi na Afisa wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar {ZEC } Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu
Khamis hapo ilipo ofisi hiyo Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
 
Akikabidhi fomu hizo Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya
Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis amethibitisha kwamba Balozi Seif
Ali Iddi ni Mgombea  halali wa kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Jimbo la Mahonda kupitia CCM.

 

Nd. Makame alisema kwamba uhalali huo unatokana na Ofisi yake kupokea
barua rasmi kutoka Chama cha Mapinduzi { CCM } iliyoainisha na
kuthibitisha kwamba Balozi Seif Ali Iddi ameteuliwa na chama hicho
kuwania nafasi hiyo ya Uwakilishi kwenye Jimbo la Mahonda.
 
Afisa Uchaguzi huyo wa Wilaya ya Kakaskazini B alifafanua na kuwataka
wagombea wote watakaochukuwa fomu za kuwania nafasi hizo kutumia fursa
ya kufika kwenye Ofisi hiyo kwa kupata ushauri zaidi wa namna ya
kujaza vyema fomu hizo licha ya kupatiwa maelezo ya awali wakati
wanapokabidhiwa.
 
Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itatoa fursa pana ya kutatua
changamoyo zinazoweza kujitokeza  na  kuepukwa mapema ili kukidhi
matarahio yaliyopangwa na tume hiyo.
 
Balozi Seif Ali Iddi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kitope kupitia chama
cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo kutokana na
mabadiliko yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  jimbo hilo
limevunjwa na kuzaliwa majimbo mawili ya Mahonda na Kiwengwa.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni