.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 31 Agosti 2015

MASPIKA WA MABUNGE DUNIANI WAKUTANA UMOJA WA MATAIFA

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda akiwa katika Mkutano wa Kumi wa Maspika Wanawake uliofanyika kwa siku mbili hapa Umoja wa Mataifa, Mkutano wa Maspika Wanawake, umetangulia Mkutano wa Nne wa Maspika zaidi ya 180 unaoanza leo jumatatu hapa Umoja wa Mataifa.
Maspika Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa IPU Bw. Choedhury Saber na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong wakati wa mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jumamosi na jumapili, ukitangulia mkutano wa nne wa Maspika wa Mabunge.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano uliojadili mbinu za kuchagiza usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya Beijing pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa malengo 17 ya Maendeleo Endelevu Baada ya 2015.


                                                                                  Na Mwandishi Maalum, New York

Mkutano wa Nne unaowakutanisha Maspika 180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi 140, unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkutano huu wa siku tatu na ambao umeandaliwa na Chama cha Mabunge Duniani ( IPU), utafunguliwa na Rais wa IPU Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matafa, Ban Ki Moon.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu. Mkutano ambao Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana na changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa maono ya Kibunge.

Mkutano wa Nne wa Maspika, ulitanguliwa na Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na Jumapili). Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda ameshiriki kikamilifu na kuongoza baadhi ya mikutano.

Mkutano wa Nne wa Maspika ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya Maspika hao na ambayo imekuwa ikifanyika kuelekea Mkutano wa Kilele wa Viongozi wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika wiki chache zijazo ambapo watapokea na kupitisha Ajenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015.


                                                                                               Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni