.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Agosti 2015

MGOMBEA URAIS WA CHADEMA, MH. EDWARD LOWASSA NA MGOMBEA MWENZA WAKE, JUMA DUNI WASAINI HATI YA KIAPO

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es
Salaam ili kuthibitisha usahihi wa fomu hizo kabla ya mkuzirejesha Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, kwa uteuzi. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Juma Haji
Duni, maarufu kama “Babu Duni”
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
hicho, Mh. Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (mbele) wakati wa kusaini fomu za hati ya Kiapo, leo Agosti 19, 2015. Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Mabele Marando.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni