.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 22 Agosti 2015

MH. LOWASSA NA MGOMBEA MWENZA WAKE, JUMA HAJI DUNI WARUDISHA FOMU TUME

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Picha na Othman Michuzi
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine waliowasindikiza, wakitoka kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi baada ya kurudisha fomu leo Agosti 21, 2015.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni