Moto bado unauwaka katika maeneo
yaliyotokea milipuko mikubwa katika mji wa Tianjin nchini China, hata
baada ya kupita saa 36.
Timu ya wanajeshi wataalam wa
kemikali inafanya vipimo vya gesi yenye sumu katika eneo hilo na
waokoaji wameagizwa kuvaa nguo za kujikinga.
Watu wapatao 50 wamekufa katika
milipuko hiyo na mamia kujeruhiwa, 71 wakijeruhiwa vibaya katika
milipuko hiyo iliyotokea jumatano jioni. Aidha kunataarifa za
kupatikana watu waliohai kwenye vifusi hii leo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni