.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 5 Agosti 2015

MSAADA ZAIDI WATOLEWA NA TBL MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI


Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ekimu kwa Umma cha Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Abel Swai sehemu ya fulana 3,800, kofia 2,800 na stika kwa ajili ya Maadhinisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyoayoanza Agosti 3 hadi 7 jijini Tanga. TBL imedhamini maadhimisho hayo kwa sh. mil 124, ambapo madereva wa masafa marefu watapimwa afya zao pamoja na kuwapatia mafunzo waendesha bodaboda 300. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.


Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ekimu kwa Umma cha Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani,Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Abel Swai moja ya vyeti watakavyokabidhiwa madereva wa masafa marefu watakaopimwa afya zao wakati wa Maadhinisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyoanza Agosti 3 hadi 7 jijini Tanga. TBL imedhamini maadhimisho hayo kwa sh. mil 124, ambapo pia mafunzo yataendeshwa kwa bodaboda 300. Makabidhiano hayo ya stika, fulana na kofia na vyeti yalifanyika Dar es Salaam.
                   Makasha yenye kofia, fulana na stika yakipakiwa kwenye gari la Polisi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni