Mtu mwenye silaha amemuua mwandishi
wa habari Peter Julius Moi kwa kumpiga risasi mara mbili mgongoni
katika Jiji la Juba, familia yake imethibitisha baada ya kutambua
mwili wake.
Moi anakuwa mwandishi wa saba
kuuwawa nchini Sudani Kusini kwa mwaka huu, wakati machafuko ya wao
kwa wao yakiendelea.
Mauaji yake yametokea siku chache tu
kupita tangu rais Salva Kiir kutishia kuua waandishi wa habari ambao
wanaandika habari za kuikosoa serikali.
Hata hivyo msemaji wa rais amesema
matamshi ya rais Kiir hayakueleweka vizuri, na polisi wameanza
uchunguzi wa kifo cha Moi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni