Mwanaume mmoja ambaye amejulikana
jina moja la Reginald, mkazi wa Karatu, amekutwa asubuhi akiwa
amefariki, ndani ya hoteli ya A Square Belmont, iliopo katikati ya
Jiji la Arusha, huku baadhi ya viungo vyake vya kichwa, sehemu za
siri, viganja vya mikono na matiti vikiwa
havipo na kuachwa kiwili wili kikiwa
hakina nguo yoyote.
Akizungumza leo, katika eneo la
hoteli hiyo, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Levolosi, Sauda
Haruna, amesema kuwa yeye alipata taarifa za kifo hicho toka kwa
Mjumbe wa serikali ya mtaa Mary Shayo na aliamua kufika eneo la tukio
na kukuta kifo hicho cha kusikitisha.
Sauda ameomba unyama huo usifanyike
tena katika Mkoa wa Arusha na wenye hoteli wahakikishe wanaandikisha
wageni wao taarifa muhimu, ili kuweza kuwatambua linapotokea tatizo
kama hilo.
Amesema marehemu inakuwa ngumu
kufahamu mkazi wa wapi, jina lake kamali kwa sababu hata namba ya
simu aliyoandika ikipigwa anapokea mtu mwingine na anashangaa
kuulizwa taarifa asizofahamu.
Kwa upande wake Isike Hamisi,
amesema yeye ana ndugu yake alilala katika hotel hiyo jirani na
chumba cha marehemu, lakini ahakusikia chochote na asubuhi alishangaa
kuambiwa chumba cha jirani kuna mauaji.
Amesema ni vema hoteli kubwa kama
hiyo wafunge kamera za CCTV ili tukio linapotokea inakuwa rahisi
kuwafahamu wauaji, tofauti na sasa inavyokuwa ngumu na cha
kusikitisha hata damu katika chumba cha marehemu hazikuwepo.
Kwa upande wa mashuhuda wa eneo la
tukio, ambao majina yao hawakutaka kutaja hadharani, wamedai kuwa
marehemu huyo anafahamika mkazi wa Mianzini na muuza mabegi, ila jina
lililoandikwa katika kitabu hicho sio la kweli.
Hata hivyo kumpata msemaji wa hotel
hiyo haikuwezekana baada ya polisi kusomba wafanyakazi wote, waliopo
katika hotel hiyo na kuwapeleka polisi kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha
Liberatus Sabas, alipotafutwa kwa njia ya simu, amesema kwa sasa yupo
mbali na ofisi na atatoa taarifa hizo baadaye.
Mwili huo umetolewa katika hotel
hiyo majira ya saa 5:45 kupelekwa mochwari na gari la Polisi lenye
namba za usajili T.422 AGA, huku umati mkubwa wa watu ukiwa
umezingira eneo la tukio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni